HATIMAYE mwili wa aliyekuwa mwimbaji na mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha Madinda umezikwa jioni hii katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar wamejitokeza na kuhudhuria maziko ya msanii huyo aliyefariki dunia juzi. Mungu ailaze roho ya marehemu AISHA MADINDA mahali pema peponi. AMEN.
Mwili wa Aisha Madinda ukiswaliwa kabla ya maziko huko Kigamboni jijini Dar hivi punde.
Mwili wa Aisha Madinda ukiswaliwa kabla ya maziko huko Kigamboni jijini Dar hivi punde.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Aisha Madinda kuelekea makaburini.