| Pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia akizungumza na waandishi wa habari |
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa Viongozi Mbalimbali wa Vyama vya Kisiasa pamoja na Wananchi wakiwalahumu Watendaji wa Serikali kwa kufanya makosa na kupelekea kuwepo na Dosari nyingi kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa ulimalizika Mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nayo Serikali imeibuka na kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali nchini na wengingine ikiwasimamisha kazi kutokana na uzembe waliofanya uliopelekea kuwepo na dosari nyingi kwenye uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.
Hayo yametangazwa leo Jijini Dar es Salaam naWaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Ghasia wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo aliwataja Wakurugenzi waliosimaishwa kazi kutokana na Udhembe huo ni Felix T.Mabula-kutoka Hamalshauri,,Fourtunatus Fwema Halmashauri ya Mbulu,Bi Isabella D,Chilumba kutoka Halmashauri ya Ulanga,Bi Pendo Malabeja kutoka Kwimba pamoja na Wiliam Z Shimwela kutoka Sumbawanga.
| Waandishi Wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakimsikiliza Hawa Ghasia leo jijin Dar |
Waziri Ghasia aliwataja tena wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na kupelekea Dosari hizo ni Bwana Benjamini A Mojoro ,Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji Mkuranga,Abdalla Ngodu,mkurugenzi Mtendaji wa Hamalshauri ya Kaliua,Masalu Mayaya,mkurugenzi wa Kasulu,Bibi Goody Pamba mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti,Julius A madiga kutoka Sengerema na Simon CR Mayeye mkurugenzi Mtendaji wa Bunda.
Vilevile,Waziri Ghasia alisema Serikali pia imewapa Onyo kali ikiwemo na kuwaweka chini ya Uangalizi na kama ikibainika wana udhaifu Mwingine Serikali haitosita kuwachukulia hatua ambao ni
Mohamed A.Maje kutoka Halmashauri ya Rombo,Hamis Yuna kutoka Halmashauri ya Busega pamoja na Jovin A Jungu kutoka Halmashauri ya Muheza.
Hatahivyo,Waziri Ghasia aliwataja pia Wakurugenzi waliopewa onyo tu ni Isaya Mngulumi kutoka Manispaa ya Ilala,Melchizedeck Humbe kutoka Manispaa ya Hai pamoja na Wallace J Karia kutoka Mvomero.
Ambapo waziri Ghasia alisema uamuzi huo wa kuwafukuza watendaji hao umetokana na ripoti alizopokea kuhusu masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi huo wa serikali za mtaa na na kwenda kinyume na sharia ya Ibara ya 36 (1) (4) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Rais ameridhia kuchukuliwa hatua hizo, ambapo pia alisema ni dhahiri kuwa wakurugenzi wa Halmashauri hizo -
Wameonesha Udhaifu mkubwa katika kutekeleza Jukumu la Usimamizi wa Uchaguzi ambalo ni moja ya majukumu ya ukurugenzi.
Alizitaja Kasoro walizofanya Wakurugenzi hao ni Kuchalewa kuandaa Vifaa vya kupigia kura,kukosa umakini katika kuandaa Vifaa hasa karatasi za kupigia kura na zengine kuwa na Makosa,Kuchelewa kupeleka -
Vifaa kwenye vituo vya kupigia kura,Uzembe katika kutekeleza Majukumu yao pamoja na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi wa uchaguzi kuwa yamekamilika.
Katika Hatua Nyingine Waziri Ghasia aligoma kujiuzulu na kusema hatua alizochukua ni wazi kwa wale waliohusika na akalitaka Gazeti la Tanzania Daima kuandika Habari za Ukweli na kuacha kudanganya Umma.
“Kiukweli nimeshangaa sana na Gazeti la Tanzania Daima la Jana kusema eti CCM imepoteza zaidi ya Asilimia 80 Mkoa wa Mtwala,jamani kusema ukweli mimi ni Mbunge kutoka huko ,Halmashauri zote za Mtwala CCM imeongoza kwa kishindo kikubwa inakuwaje Mwandishi tena uliosomea kuandika habari ya uongo kiasi hicho”
“Na hili sijui mwandishi wa Gazeti hili alikuwa anamaanisha nini na kama huyo Mwandishi wa Gazeti hili angekuwa mtendaji wangu ningemwajibisha kwa kupotosha Umma”alisema Waziri Ghasia