BPESA YAJITANUA ZAIDI KUPITIA I&M BANK
Dar es Salaam 17thDec, 2014
BPESA leo imetangaza ushirikiano mpya kati yake na benki ya I&M kwa kuzindua kadi mpya ya BPESA EMV pamoja na PIN card ikiwa na lengo la kusambaza huduma kwa wateja wake na kwa Watanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi mkuu wa B Pesa, Sean Merali, akiongea na wageni waalikwa hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa ushirikiano mpya kati ya B Pesa na I &M benki ,ambapo ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa kuwafikia wateja wao kiurahisi kwa taasisi hizo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikua ni kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam , Suleiman Kova. Katika halfa iliyofanyika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam.
Wateja wa BPESA wanaweza kuweka au kuchukua fedha zao kupitia matawi yoyote ya benki ya I&M ambayo yanapatikana nchi nzima.
BPESA inatoa fursa kwa wateja wake kupitia njia mbalimbali za kielectroniki kama vile web portal au njia ya vifaa simu kwa njia ya programu za Android na USSD kutumia kadi zao BPESA . kadi za BPESA zinaweza kujazwa katika maduka yote ya EzyPesa baada ya makubaliano na Zantel ambayo yalifanywa mwanzoni mwa wiki hii.
Mkurugenzi mkuu wa B Pesa, Bw.Sean Merali,(kushoto) Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, wa pili kushoto , na mkurugenzi wa I & M Banki , Michael Shirima, wa tatu toka kushoto, na Shameer Patel, Meneja mkuu wa I & M Benki wa pili kushoto wakikata keki kama ishara ya uzinduzi wa ushirikiano mpya kati ya B Pesa na I &M benki ,ambapo ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa kuwafikia wateja wao kiurahisi kwa taasisi hizo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikua ni kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam , Suleiman kova, hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam.
BPESA ni kampuni ya kwanza naya kipekee kuanzisha huduma ya haraka kwa wafanya biashara wakati huo huo ikiboresha huduma ya kadi. BPESA pia ina mfumo wa lugha mbalimbali kwa masaa 24 kwa siku 7 katika vituo mbalimbali vya huduma nchini Tanzania kwa ajili ya maajenti wanaotumia lugha ya Kiswahili, Kingereza na Kihindi
BPESA imefanikiwa kuleta mabadiliko katika secta ya huduma ya kifedha kwa kuleta urahisi kwa watu walio au wasio na akaunti za benki kufanya miamala au kufanya malipo mbalimbali pasi na kuwa na fedha taslim mkononi. Hii ni njia salama na rahisi Zaidi kwa mtu kubeba na kutumia pesa ambapo BPESA hutoza kiwango cha chini cha huduma ya muamala.
baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa ushirikiano wa B Pesa na I & M Benki wakisikiliza mgeni rasmi kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova hayupo Pichani , wakatio wa hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serene jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, katika hoteli ya Serena Jijini Dares salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa BPESA, Bwana. Sean Merali alisema kwamba uhusiano kama huu ni muhimu kwa benki nyingine za Afrika Mashariki katika soko hili ambalo limekuwa likibadirika hasa ukizingatia kwamba uhitaji wa huduma bora na za teknolojia mpya zimekuwa zikihitajika sana na wateja wetu‘’
Bwana. Merali aliongeza kwamba wako katika hatua za mwisho kuzindua huduma ya kadi za BPESAna kenki ya Stanbic Bank pamoja na benki ya DTB, zote zikiwa zimepata uthibitisho kutoka Benki kuu ya Tanzania.