Polisi wakikabiliana na waamdamanaji waliotaka kuingia bungeni jijini Hong Kong leo.
Baadhi ya silaha walizotumia waandamanaji kujaribu kuingia bungeni.
VURUGU zimezuka kati ya polisi na kundi dogo la waandamanaji
waliokuwa wakitaka kuingia bungeni asubuhi hii jijini Hong Kong nchini
China.Baadhi ya waandamanji hao wakiwa wamevaa mask walitumia vyuma kujaribu kuvunja mlango mmoja wa pembeni wa bunge kabla ya kudhibitiwa na polisi walioamua kutumia maji ya kuwasha kuwatawanya.
Takribani wiki nane sasa waandamanaji wamekuwa wakiandamana kudai demokrasia katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo la Hong Kong.