Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa
kutoa huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye
alikuwa anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na
wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopita
Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.
Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.
Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.
Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.
