Home » Uncategories » MAHARUSI WAOANA NDANI YA BWAWA LA MAJI
Tuesday, November 25, 2014
MAHARUSI WAOANA NDANI YA BWAWA LA MAJI
Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .
Bwawa hilo hutumiwa kutoa mafunzo ya kupiga mbizi katika kituo cha Fort William. Bi
Dorota Bankowska mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni
mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi jana lakini
akataka sana kufanya jambo la kipekee wanakoishi kama ishara ya
kusherehekea harusi yao.
Bi
Abbott alipokea mafunzo ya upigaji mbizi katika kituo hicho kilicho
katika ufuo wa bahari ya Loch Linnhe mnamo mwaka 2007 na kuwaomba
wafanyakazi wa kituo hicho wamruhusu afanye harusi yake chini ya maji
hayo.
Bwawa hilo, hutumiwa kutoa mafunzo kwa wapiga mbizi pamoja
na kufanyia majaribio vifaa vipya. Picha hizi zimetolewa na kituo hicho.
Bi harusi alivalia gauni nyeupe huku bwana harusi akivalia sketi ambayo huvaliwa na waskochi ijulikanao kama 'Kilt'.
Maharusi hao waliungana na marafiki wao Ala Bankowska na Charlie Cran-Crombien chini ya maji hayo.
Wote wanne walivalia vifaa vya kupigia mbizi pamoja na mavazi yao ya harusi.
Takriban wageni 100 walitazama harusi hio wakiwa nje
Bi Abbott anafanya kazi katika kiwanda cha mafuta na gesi.