|
Doreen Kabuche |
“Mwaka 2011 Doreen Kabuche alimaliza Kidato cha sita Benjamin Mkapa na
kuwa best female student. Tulimwita na nikamzawadia laptop ya 1,500,000
Mwaka huu amekuwa best student UDSM kwa kupata GPA 4.8 kwenye shahada
adimu ya takwimu bima. Nataka tumsomeshe Masters ili kupata wataalam
wataoangalia mifuko yetu ya pension Tuache kulalamikia utendaji mbovu
wakati hatusomeshi wataalam” , ni maneno ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Ilala, Jerry Silaa alipokuwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari
wakati wa kumpongeza mwanafunzi Doreen Kabuche aliyemtembelea ofisini
kwake leo.
|
Jerry Silaa |