Wengi wamehoji kwanini mwanamume huyu amejikata uume wake badala ya kwenda hospitali kwa upasuaji
Msanii
Mrusi aliyecheza katika filamu mashuhuri ya 'Burnt by the Sun 2',
alipoteza uume wake baada ya kujikata akitaka kuwa mwanamke.
Kikubwa kilichomfanya msanii huyo Evgniv Sapaev kujitaka sehemu zake za siri ni kwamba alitaka sana kuwa mwanamke.
Mwanamume
huyo alionekana akotoka nje ya nyiumba yake huku damu ikimwagika kutoka
kwa sehemu zak nyeti kufuatia upasuaji aliojifanyia mwenyewe.
Msanii
huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye nyota yake ilikuwa inang'ara sana
alikimbizwa hospitalini kwa huduma ya dharura kwa hofu ya hali yake kuwa
mbaya .
Madaktari walijaribu kumshona lakini hawakufanikiwa katika juhudi zao za kumrejeshea mwanamume huyo uume wake.
Afisaa
mmoja hospitalini ambako muigizaji huyo alipokea matibabu alisema
alikuwa na bahati sana kuponea kwani alivuja damu nyingi na kwamba
angepoteza muda kidogo tu angefariki.
Kwa mujibu wa jarida la
Mirror, jirani ya Evgniv Sapaev, Arkhip Tikhonov mwenye umri wa miaka 57
alishtuka sana alipombishia mlango na kujionea hali yake akiwa tayari
ameanza kudhoofika kwani alikuwa amepoteza damu nyingi sana.
''Alionekana
akitisha sana akiwa na damu mikononi mwake huku akishika sehemu yake ya
uuma ambayo alikuwa ameikata. Nilidhani alikuwa anafanya mazoezi ya
uigizaji, lakini alipozirai mlangoni huku akiwa ameshika sehemu yake ya
siri mkooni ndipo nilipogudnua kuwa mambo yalikuwa mbaya,'' alisema
jirani wa Evgniv
Baada yua kupata nafuu mwathiriwa alinukuliwa
akisema, ''tangu niwe mtoto mdogo nimekuwa nikijihisi kuwa mwanamke.
Nilijaribu mara nne kukata nyeti zangu lakini wakati wote sikuwa na
ujasiri wa kufanya hivyo.Lakini wakati huu niliweza kufanya hivyo baada
ya kumeza tembe za kuzuia maumivu, na kujitaka kwa kutumia kisu.
Badhi walimkosoa msanii huyo kuwa kujikata sehemu zake za isiri badala ya kwenda hospitalini kwa upasuaji.
