Kioo cha lori cha mbele kikiwa kimepasuka.
Makreti ya soda yalivyoanguka.
Baadhi ya kreti za soda zikiwa zimezagaa eneo la ajali.Mmoja wa wahusika akitoka kuzima na kuuchomoa ufunguo wa gari lililopata ajali.
Askari wa JWTZ wakilinda usalama wa eneo hilo baada ya ajali kutokea
Askari wa usalama barabani wakikagua ajali
Vinywaji mtaroni
Sehemu ya foleni inayosababishwa na gari hilo.
WATU watatu akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca
Cola walipata michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo ya
Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa mashuhuda amesema
chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari
hilo kubwa lililokuwa limebeba vinywaji na ndipo gari kubwa likiwa
katika kukwepa likajikuta likianguka ubavu.
