STURRIDGE AMESAINI MKATABA MPYA NA LIVERPOOL



Straika wa Liverpool  Daniel Sturridge amesaini mkataba mpya  katika klabu hiyo.
Sturridge ambaye amesain mkataba mrefu wa miaka 5 utakaodumu hadi majira ya joto 2019 alijiunga na Majogoo wa Anfield mwaka 2013 akitokea  Chelsea kwa dau la EURO 12M Na kuwa chaguo la maneja  Brendan Rodger katika kikosi cha kwanza cha liverpool.
Hadi sasa Sturridge amefunga magoli 36 katika mechi 50 za mwanzo na kumfanya kuwa mfungaji bora wa Liverpool katika mechi 50 za mwanzo zaidi ya miaka 100.