Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo (JANA) usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Baadhi ya watoa mada mbalimbali
katika semina hiyo wakiwa meza kuu
Baadhi ya Vijana walioitumia
Fursa ya kutengeneza fulana za tamasha la Fiesta baada ya kubaini kuna uhaba
mkubwa wa fulana hizo,ambazo zilitarajiwa kusambazwa na waandaji wenyewe,Vijana
hao waliuza fulana hizo kila moja kwa shilingi Elfu kumi kwa kila moja.
Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa wamenyoosha mikono juu wakiunga mkono moja ya mada iliyokuwa ikizungumza kwenye semina hiyo iliyofanyika katika moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
Muonekano wa ukumbi mlimofanyika
semina ya Fursa 2014 mapema leo asubuhi.
Baadhi ya Washiriki wa Semina ya
Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa ndani ya ukumbi wa hoteli ya
KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikizungumzwa.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa
Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa
Namfua mjini Singida.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka
kundi la Hip hop lijulikanalo kwa jina la WEUSI,Niki wa Pili akizungumza mbele
ya mamia ya washiriki wa semina ya fursa iliyofanyika katika hoteli ya KBH nje
kidogo ya mjini wa Singida,Niki amewataka vijana mbalimbali kuhakikisha ndoto
zao haziishii njiani na badala yake wazifanyiekazi ili kujiletea maendeleo
katika maisha yao ya kila siku,pia amewataka kuitumia vyema fursa wanayoipata
katika njia mbalimbali.v
Mmoja wa washiriki wa semina ya
Fursa,akiulaza swali na pia kuielezea fursa aliyonayo katika harakati za
kutafuta maendeleo.
Mkurugenzi wa kampuni ya
Automobile Garage,Joseph Msuya akifafanua jambo kuhusiana na namna
alivyoaianzisha kampuni yake na kufikia hapo alipo,akitumia teknolojia za
kisasa kabisa katika suala zima la ufundi wa magari,utengenezaji Viyoyozi vya
magari na mambo mengine mbalimbali.






