Mamia
ya watu kwa shangwe na vigelegele wamemkaribisha Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta baada ya kurejea kutoka kikao chake katika mahakama ya
kimataifa ya ICC mjini the Hague.
Kenyatta alihudhuria kikao
maalum katika mahakama hiyo Jumatano, na kuwa Rais wa kwanza aliye
mamlakani kufika katika mahakama hiyo.Mahakama hiyo ilimtaka afike mbele yake kutokana na malalalmsihi kutoak kwa kiongozi w amashitkaka kuwa serikali ya Kenya inaficha ushahihidi kuhusiana na kesi inayomkabili.
Kenyatta alipokelewa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanacheza densi pamoja na gwaridde la heshima.
Asubuhi na mapema, wafuasi wake walipanga foleni kwenye barabara ya kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Nairobi.
Rais aliwahutubia kwa mda mfupi umati huo wa watu ambao waliombwa kufika kumpokea rais na waziri wa usalama.
Mwandishi wa BBC aliyefika kushuhudia Rais huyo akiwasili nchini alisema kuwa Kenyatta ana wafasui wengi


