KWA WALIO KOSA TUKIO LA MISS TANZANIA NI HUYU HAPA....

Miss Tanzania 2014, Siti Abbas Zuberi Mtemvu akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililoshirikisha warembo 30 na kufanyika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Siti Mtemvu ametwaa taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Happyness Watimanywa.

Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa kwanza Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
Picha zote na Othman Michuzi.