Ugonjwa wa ukimwi uligunduliwa miaka ya 1920 mjini Kinshasa, nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo. Wanasayansi wameeleza.
Wanasayansi
wa kimataifa wanasema ongezeko la watu,vitendo vya kukutana kimwili na
shughuli za usafirishaji kwa njia ya reli zilifanya virusi vya ukimwi
kuenea.
Ripoti inasema kuwa biashara ya ngono, ongezeko kubwa la
watu na vitu vyenye ncha kali kama sindano kwenye zahanati huenda
kulichangia kusambaa kwa ugonjwa huo DRC.
Wakati huo huo reli
ilikuwa ina watu takriban milioni moja waliokuwa wakiingia na kutoka kwa
wingi jijini Kinshasa kwa mwaka,wakisambaza virusi kwenda kwenye miji
mingine.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga.
Ukimwi ulitambulika kuwa janga kimataifa mwaka 1980 na uliathiri takriban watu milioni 75.
Ugonjwa huu una historia ndefu barani Afrika , lakini ulipotokea ugonjwa huu bado ni mjadala mrefu.
Timu
ya wanasayansi kutoka chuo cha Oxford na chuo cha Leuven, nchini
ubelgiji walitafiti chanzo cha ugonjwa wa ukimwi wakisema kuwa ulianzia
kwa Sokwe.
Virusi vya HIV ni sawa na virusi vinavyopatikana kwa
Sokwe ambavyo vinajulilkana kama Simian ambavyo vinadhaniwa vilitoka kwa
Sokwe na kuambukizwa binadamu kupitia kwa damu wakati wakitafuta nyama
ya wanyamapori.
Virusi hivyo vilikuwa na muundo tofauti na muundo
huo ulikuwa unabadilika kila wakati. Virusi vya kwanza viliwaathiri
maelfu ya watu nchini Cameroon.
Virusi vilisambaa kwa kiasi kikubwa, mpaka nchi jirani ya Congo Brazzaville na katika maeneo ya migodi, katika jimbo la Katanga
Idadi kubwa ya wanaume waliokuwa wanafanya kazi mijini na idadi ya
wanaume ndio ilikuwa kubwa kuliko wanawake na hivyo biashara ya ngono
ikawa kubwa sana.
Mmoja wa watafiti Profesa Pybus anasema kuwa
mambo mawili yanesaidia kupunguza maambukizi. Kwanza hamasisho la
serikali kuwatibu wagonjwa kwa maradhi tegemezi.
Jambo la pili
ingekuwa mfumo wa usafiri ambao uliwawezesha watu kusafiri kutoka sehemu
moja hadi nyingine huku ugonjwa ukienezwa zaidi.
Takriban watu milioni moja walikua wakitumia reli ya Kinshasa mwishoni mwa mwaka 1940.
Virusi
vielendelera kuenezwa kwa nchi jirani ya Brazzaville na mkoa wenye
madini wa Katanga ambao ulikuwa kitovu cha ugonjwa huo.
Virusi havikukomea tu nchini Congo bali vilianza kuenezwa kote duniani


