JAMBAZI SUGU ALIYEKUWA AKIUA WANAWAKE ARUSHA AUAWA



Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Ramadhan Abdallah Jumanne, ambaye amekuwa akiwaua kwa kuwapiga risasi wanawake mbalimbali jijini Arusha, ameuawa katika mapambano ya kurushiana risasi na Polisi.

Wadau habari zilizovuma siku chache jijini Arusha ni matukio yenye kufanana ya kuporwa,kujeruhiwa na hata kuuawa kwa wanawake mkoani Arusha.

Matukio haya yaliwastua wengi sana kwani haikujulikana wazi kuwa ni ujambazi,visasi ama mauaji ya kupanga lakini habari za hivi punde ni kwamba mpanga matukio hayo yote (master mind) ameuawa na jeshi la polisi eneo la Moivo Sanawari ya juu na hivi sasa wananchi wamejazana kituo kikuu cha polisi Arusha wakiutizama mwili wa muuaji huyo aliyeikosesha Arusha raha kwa muda sasa.