Wednesday, October 01, 2014
MAREKANI YASHAMBULIA ISIS LICHA YA ONYO
|

Mwandishi wa Marekani aliyeuawa na kundi la ISIS |
Thursday, August 21, 2014 6:11 PM
Majeshi
ya Marekani yameendelea kuwashambulia wapiganaji wa Islamic State huko
Iraq licha ya vitisho kutoka kwa kundi hilo kuwa watawaua mateka wengine
wamarekani iwapo Obama angeendelea kuishambulia himaya hiyo kaskazini
mwa Iraq. |
Majeshi ya Marekani kwa ushirikiano na ndege zisizikuwa na marubani zilifanya mashambulizi 14 usiku wa kuamkia leo. Mashambulizi
kumi na manne ya angani yamefanyika katika eneo karibu na bwawa la
Mosul na yalilenga kuwasaidia wanajeshi wa Iraq na wa kikurdi.
Bwawa la Mosul lililotekwa kutoka kwa wapiganaji wa IS Maafisa
wajeshi la Marekani wamesema kuwa walifaulu kulipua magari ya kijeshi
na vitu vingine vilivyokuwa vikitumiwa na wapiganaji wa IS . Tarifa
kutoka kwa wakurdi zinasema kuwa ndege ambazo hazina rubani zilikuwa
angani kuwalinda wanajeshi Wakurdi wakati wapiganaji wa Pesh Merga
wakisukumwa katika milima, kusini mashariki mwa bwawa kubwa la Mosul,
ambalo lilitwaliwa tena kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu wiki hii. Pentagon
imethibitisha kuwa mashambulizi kumi na manne ya angani yalifanywa
katika sehemu hiyo kuliko bwawa na kuyalenga magari kadhaa ya kijeshi na
vitu vingine. Televisheni ya taifa ya Iraq imesema kuwa ndege hizo
za vita za Marekani zilikuwa pia zimetekeleza mashambulizi katika kambi
za magaidi mkoani al-Anbar hadi magharibi mwa Baghdad, na zilikuwa
zimetoa ulinzi wa angani kwa vikosi vya serikali vilivyokuwa vikielekea
kuwakabili waasi wa kisuni.
Majeshi ya Iraq yakielekea kukabiliana na wanamgambo wa Islamic State Awali
makao kuu ya Jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi la kitengo
maalum walijaribu kumuokoa mwanahabari James Foley na waamerika wengine
walioshikwa mateka nchini Syria. Habari hii imetolewa baada ya video
ya aliyetekwa nyara novemba 2012 nchini Syria kuonyeshwa akiuawa
kikatili na wanamgambo wa Kiislamu kutokea jumapili . Wanamgambo hao
walisema mauaji yake ilikuwa kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kwa
sababu ya kuwashambulia wapiganaji wao hewani Iraq.
Rais wa
Marekani Barack Obama alikashifu mauaji hayo na kuwalinganisha
wanamgambo hao na ugonjwa wa saratani na kuwa itikadi zao hazikuwa na
mwelekeo aliendelea kuwa kusema tendo hilo lilishtua ulimwengu mzima
Umoja wa kitaifa ,uingereza na wengine pia wameeleza huzuni yao kutokana na video hiyo. Mamake Bwana Foley Diane alisema kuwa mwanawe aliaga dunia kwa niaba ya watu wa Syria. Kamati
inayolinda wanahabari ilisema ina wasi wasi kwa wanahabari wote
waliozuiliwa na wanamgambo hawa na kusema wanahabari wajiepushe na
Syria. |