Ukivunja sheria, uhusiano mzuri utakosa - BASATA



Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha east Africa Radio, Afisa habari wa BASATA Artides Kwizela, amesema wao kama chombo cha serikali kazi yao ni kuratibu kazi za wasanii, na iwapo zimeenda kinyume lazima litaingilia kati, kwani uhusiano mzuri hauwezi kukaa kimya pale mambo yanapokwenda kinyume.

"Linapokuwa limetokea suala fulani BASATA inaiunuka inasema no, ni kwa sababu kunakuwa kuna mambo fulani hajaenda sawa, na sisi kazi yetu kama BASATA ni kuratibu sekta ya sanaa, ni kuhakikisha kila kitu kwenye sekta ya sanaa kinakwenda kwa utaratibu, kwa hiyo kunyoosheana kidole au BASATA kusimama na kusema no, ni kwasabau kunakuwa kuna taratibu fulani hazijafuatwa, kwa hiyo kitu ambacho ni cha msingi uhusiano wowote ule hauwi uhusiano unaelekeza kwenye kuvunja sheria", alisema Bwn. kwizela.




Pamoja na hayo BASATA imesema wasanii wanatakiwa kutumia ubunifu zaidi katika kufikisha ujumbe wao, na sio kwa kutaja majina na kutumia lugha chafu, ili kufikisha ujumbe wao kwa hadhira.

"Sanaa ni ufundi ni ubunifu, na katika vitu ambavyo ni vya wazi ambavyo msanii lazima avizingatie ni matumizi tu ya lugha ya picha ya kawaida lakini linafikisha ujumbe, sio lazima ufikie hatua ya kutaja majina ya watu na kuwatukana watu ndio ufikishe ule ujumbe mzuri", alisema Bwn. Kwizela.