Maarufu Bongo, Amri Athumani ‘King Majuto au Mzee Majuto’.
Kila mtu na mtoko wake, mchekeshaji maarufu Bongo, Amri Athumani ‘King Majuto au Mzee Majuto’ anatengeneza mkwanja mrefu kwa kuwavunja mbavu watu.
Leo ndiye ana husika katika makala yetu ya utajiri na utapata kujua ni vitu gani anavyomiliki kupitia sanaa yake hiyo.
Toyota Noah
Mzee Majuto: “Kuna siri nyingi za kufanikio lakini kubwa ni kutokubali kukatishwa tamaa hata kama kile unachokipata ni kidogo. Ni kweli kupitia sanaa ya uchekeshaji nimepata mafanikio lakini ni baada ya kupitia msoto mkali.
MASHAMBA
“Kwa kuwavunja mbavu watu, ninamiliki mashamba yenye ukubwa wa heka 8 hivi. Pia nimeweza kusimama na kundi langu la Majuto Unity lenye wasanii zaidi ya 50. Kwangu mimi haya ni mafanikio makubwa.
MATANGAZO
“Nimekuwa mtu wa kujituma sana, ninafanya matangazo mengi ya bidhaa mbalimbali za chakula na mengineyo.
Nissan Caravan
“Kwa upande wa magari nina Nissan Caravan, Toyota Hiace Custom, Noah na Kirikuu (Suzuki).
“Pia najishughulisha na ufugaji wa kuku, ng’ombe na mbuzi kama 20.
Toyota Hiace.
“Usisahau kwa kuchekesha watu, nina nyumba mbili zilizoko Tanga Mjini na nyingine kijijini kwangu.”
Huyo ndiye Mzee Majuto aliye wahi kucheza sinema zaidi ya 70 za vichekesho zikiwemo Inye Gwedegwede, Shikamoo Mzee, Ndoa ya Utata, Daladala, Nimekuchoka, Trouble Maker, Kizunguzungu, Shoe Shine, Street Girl, Mtego wa Panya, Lakuchumpa, Bishoo, Nakwenda kwa Mwanangu, Bishoo, Wizi wa Kuku, Mtu Mzima Hovyo na nyinginezo.
Suzuki Carry (Kirikuu).
Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma Shule ya Msingi ya Msambwini jijini humo. Alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka 9 kwa kuigiza majukwaani. Pia ni mtunzi, mwigizaji, mwimbaji na mwandishi wa miswada.
Hivi karibuni, Mzee Majuto alitangaza kuacha kufanya kazi za wasanii wenzake kwa maana ya kushirikishwa na kujikita zaidi katika kazi zake mwenyewe.