Soma Jinsi Tundu Lissu Alivyomlipua Magufuli Kwa Kusema Siku 100 za Ikulu Rais Amelikimbia Jukumu la Zanzibar

Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni mwanasheria wa (CHADEMA)Tundu Lissu amesema siku 100 ambazo Rais Dkt.John Magufuli kuwa madarakani amenyamaza kabisa kuhusu Zanzibar huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiwa vimeongezwa Zanzibar.




Lissu ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na EATV kuhusu tathmini yake kwa siku 100 ambazo Rais Magufuli amekaa madarakani ambapo amesema suala la ulinzi na usalama wa nchi hii linaongozwa na yeye hivyo kukaa kimya ni kukwepa jukumu lake.

''Yeye kama amiri jeshi mkuu hawezi kujitoa katika hili kwa sababu vyombo vyake ndivyo vimetoka bara kwenda huko kisiwani Zanzibar kuwanyamazisha wananchi hivyo hawezi jitoa katika suala hili kwa namna yeyote''Amesema Lissu.

Lissu ameongeza kuwa wakati vikao vya Bunge vikiendelea mjini Dodoma, Waziri Nape alitangaza kusitishwa kwa matangazo ya bunge kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na badala yake yatakuwa yanarekodiwa na kutafutiwa muda wa ziada, wakati matangazo hayo yamerushwa live kwa miaka 10

Aidha suala la kukamata makontena hatujawaona hao ambao wamakwepa kodi na hatua zilizochukuliwa wakati sheria za nchi zinasema kukwepa kodi ni kosa la jinai, pia suala la kutosafiri na kusema amekwepa gharama si kweli kwani wakuu wa mikoa,wakurugenzi na wakuu wa wilaya ni walewale na wakikwepa kutumia ndege mafuta wanayotumia kutoka Dar kwenda mikoani gharanma iko pale pale.