Mwananchi akikatiza katika mitaa ya New York, Marekani ambayo nayo imekumbwa na theluji.
Gary Utley wa Alexandria akivuta gari lake aina ya Jeep kulitoa kwenye theluji.
Wananchi wakisaidiana kunasua gari lililonasa kwenye theluji.
Mwanaume huyu aliamua kupozi kwa ajili ya ‘selfie’ juu ya theluji.
Bethany Wallace akipakia baadhi ya mahitaji yake kwenye gari huko Marstons Mills, Massachusetts.
Theluji ikiwa imetanda katika Jiji la New York, Marekani.
Wafanyakazi wa Jiji wakiondoa theluji katika mitaa ya New York.
Theluji ikiwa imetapakaa katika maeneo ya Manhattan.
Magari yakiwa yamefunikwa na theluji huko Prince William, Virginia.
Ni theluji kila kona katika mitaa iliyo mashariki mwa Marekani.
Maeneo mengi ya mashariki mwa nchi ya Marekani yamefukiwa na theluji kufuatia kuanguka kwa kiwango kikubwa zaidi cha theluji kuwahi kushuhudiwa.Zaidi ya watu milioni 80 katika majimbo 18 wameathirika. Usafiri wa reli na ndege umetatizwa na zaidi ya watu 200,000 kubaki bila umeme.
Maeneo mengine yalishuhudia theluji yenye hadi urefu wa mita moja. Utawala katika Mji wa New York unasema marufuku kuhusu usafiri inabidi kuondolewa licha ya mji huo kushuhudia theluji kubwa leo Jumapili.