Baada ya wakala wa kiungo wa Man City Yaya Toure kuthibitisha kuwa mteja wake atakuwa tayari kusikiliza ofa kutoka klabu yoyote mwishoni mwa msimu, kitendo ambacho kinaashiria kuwa kiungo huyo yupo katika mipango ya kuhama klabu hiyo, January 22 kocha wa klabu ya Man City Manuel Pellegrini ametoa kauli kuhusu kiungo huyo.
Pellegrini amemwambia au amemshauri Yaya Toure kuwa kwa sasa sio wakati wa kuwaza kuondoka anachotakiwa kufanya ni kuweka mawazo yake Man City na kucheza mpira hadi mwisho wa msimu ndio aanze kufikiria chochote kutokea “Kwa Yaya kitu muhimu kwa sasa ni kufikiria kuhusu mechi inayofuata, halafu mwisho wa msimu ndio afikirie chochote kinaweza kutokea, lakini kitu muhimu kwa sasa ni kufikiaria kuhusu msimu huu na kupambana kutwaa mataji” >>> Pellegrini
Toure ambaye anatarajiwa kurudi dimbani kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu kati ya Man City dhidi ya West Ham United baada ya ushindi wa dhidi ya Crystal Palace, anatajwa kuwa katika mipango ya kutaka kujiunga na klabu ya Inter Milan ya Italia, baada ya kumalizika kwa msimu.