Imetufikia ripoti kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar kuhusu idadi ya watu waliokamatwa na wanahojiwa na Jeshi la Polisi wakihusishwa na tukio la uvamizi wa Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar.
Kingine ni kwamba watu hao wamekutwa na vitu mbalimbali… Vitu vyote vilivyopatikana vimekutwa na Polisi eneo la Mkuranga vikiwa vimefichwa ndani ya shimo.
Tayari nimepata picha kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, silaha zilizopatikana zimeoneshwa hapa.. kulikokutwa hizo silaha kumekutwa na vitu vingine pia, ikiwemo pesa Milioni 170.

Kati ya watu waliokamatwa wapo ambao walikutwa na hizi pikipiki ambazo zilitumika kwenye tukio la uvamizi.

Kamanda wa Polisi, Simon Silo ndio anayeongoza Oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa tukio la uvamizi Kituo cha Polisi.
Source:Millard Ayo









