Vanessa Mdee 'Mimi Huwa Sisomi Maoni ya Mashabiki Mtandaoni, Wengi Wanaharibu Hali ya Hewa Kwa Matusi'>>>>






Mastaa wengi wamekuwa wakitukanwa na kupewa maneno ya hovyo katika mitandao ya jamii. Mara kadhaa maneno machafu hutolewa baada ya msanii kuandika lolote au kuweka picha.

Mshindi wa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki,Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema hana utamaduni wa kusoma maoni ya mashabiki wake, kwani alijaribu kufanya hivyo akaona yanampa msongo wa mawazo.

“Sisomi maoni ya mashabiki kwa sababu walio wengi wanaharibu hali ya hewa. Mtu utarudi nyuma kwa kuwaza mambo ya watu, ukiona Nick Minaj ameweka kitu kwenye ukurasa wake haimaanishi kwamba anapenda, ni sehemu ya kazi,” alisema.

“Nilipotaka kutumia rangi katika video yangu nilikuwa nimepanga na isitoshe ilikuwa ni wazo jipya. Sipendi kila kazi yangu ifanane na za wengine, suala la kuwa na vitu vingi linakuongezea, zile rangi mbalimbali ni wazo la watu.

Walio wengi hawakujua video hiyo wala hawafahamu rangi zilimaanisha nini,” alisema Vee Money.