BONDIA Maarufu Nchini wa Ngumi za Kulipwa, Francis Cheka Atoka Gerezani----->>





BONDIA maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kutakiwa kulipa fidia ya Sh. milioni moja kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake amebadilishiwa adhabu ya kifungo.

Cheka amechiwa na kutoka gerezani na sasa anatakiwa kutumikia kifungo cha nje.
Cheka alihukumiwa na Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya baada ya kumkuta na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro Mjini aitwaye Bahati Kabanda ‘Masika’.