.." class="size-full wp-image-91770" height="442" src="http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/02/Jay-Z-gave-Beyonc%C3%A9-sweet-grab-while-watching-US-Open-June.jpg?resize=2048%2C1415" style="border: 0px none; display: block; height: auto; list-style: none; margin: 0px; max-width: 100%; outline: none; padding: 0px;" width="640" />
Biashara hii imetokana na diet ambayo Jay na Beyonce waliifanya kwa muda wa siku 22 ambapo walikuwa wanakula vyakula vya mboga pekee.
Beyonce aliamua kuja na wazo hili la biashara baada ya kufuata mpangilio wa kula wa siku 22 ambao alifuata akiwa na mumewe Jay Z mpango ambao unasaidia kupungua uzito na kurutubisha mwili .
Jay Z alizungumzia mpangilio mpya wa chakula ambao yeye na mkewe wataufuata siku moja kabla ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliandika kwenye mtandao wa Life and Times kuwa siku moja kabla ya kufikia siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 44 ataanza mpangilio mpya wa chakula ambao utahusisha vyakula vya mboga pekee.
Hata hivyo bado haijafahamika lini biashara hii ya chakula ya Beyonce na Marco Borges itaingia sokoni .